Jumatano , 17th Dec , 2014

KOCHA wa Timu ya Taifa ya wanawake Rogasian Kaijage amesema anaamini timu yake itafanya vizuri katika mechi ya Kirafiki dhidi Zimbabwe inayotarajiwa kuchezwa kati ya Desemba 23 na 24 mwaka huu nchini Zimbabwe.

Kaijage amesema mpaka sasa timu hiyo imeshajijenga katika mazoezi yatakayoweza kuwasaidia kuwa na mawasiliano pindi wawapo Uwanjani pamoja na ushirikiano katika mchezo huo ambao anaamini utakuwa na ushindani mkubwa.

Kaijage amesema mechi hiyo itakuwa ni sehemu ya majaribio kwa ajili ya michuano ya michuano ya Afrika All Africa Games itakayofanyika hapo mwezi Mei hapo mwakani Congo Brazzaville ambapo anaamini mashindano hayo yataweza kuisaidia timu hiyo kuweza kujijenga na kufanya vizuri.