Jumatano , 7th Jan , 2015

SHIRIKISHO la Soka Ulimwenguni FIFA linatarajiwa kuanza Programu yake ya maboresho ya viwanja ambapo uwanja wa Kaitaba uliopo Mjini Bukoba utaanza kuwekwa nyasi bandia Januari 13 mwaka huu.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF, Jamal Malinzi amesema programu hiyo itasaidia kukuza na kuboresha vipaji hapa nchini.

Malinzi amesema, uwanja huyo ambao hutumiwa na timu ya Kagera Sugar ambayo inashiriki mechi za ligi kuu Tanzania Bara, utaweza kusaidia timu hiyo kuweza kufanya vizuri kutokana na ubora wa uwanja huo.