Jumanne , 16th Apr , 2024

Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni,Sanaa na Michezo Gerson Msigwa ametoa wito kwa sekta binafsi kuwekeza katika miundombinu ya viwanja vya michezo ili kusaidia kukuza michezo nchini.

Msigwa ametoa taarifa hiyo katika kongamano la uwekezaji lililohusisha wadau wa sekta ya michezo utalii ukarimu katika kujadili fursa za uwekezaji kuelekea michuano ya AFCON 2027 ambayo itafanyika kwa ushirikiano wa mataifa ya Tanzania, Uganda na Kenya.

'' Naomba ndungu zangu msiogope kuwekeza kwenye michezo kwa kujenga  na  vituo vya michezo ambavyo vina kila kitu ambavyo wachezaji wachezaji kwani serikali pekee yake haiwezi , hakuna sehemu ambao inalipa kama sekta ya michezo ''amesema Msigwa .

Nao wanamichezo walijitokeza katika kongamo hilo wamesema kuwa mashindano ya AFCON 2027 yataleta watu kutoka mataifa mbalimbali  hivyo wamesisitiza wenyeji kuwa wakarimu kwa wageni wataokuja nchini kutazama mashindano hayo.