
Anthony Joshua na Tyson Fury
Mabondia wote wawili walifikia makubaliano ya kupigana mapema mwishoni mwa mwaka jana, lakini kwa mujibu wa taarifa ni kwamba pande zote mbili zimeshasaini makubaliano ya kupigana mapambano mawili ambapo pambano hilo linatajwa kuwa na thamani ya pesa za Uingereza Pauni Milion 200 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni mia sita arobaini na tatu, kwa pesa za kitanzania, ambapo kila mchezaji atachukua zaidi ya bilioni mia tatu ishirini na moja.
Antony Joshua mwenye umri wa miaka 31, anashikilia mikanda minne WBA, WBO, IBO na IBF wakati mpinzani wake Tayson Fury anashikilia mkanda wa WBC, hivyo pambano hili litahusisha mikanda yote 4 mikubwa ya uzito wa juu kwenye mchezo wa masumbwi Duniani.
Fury kapigana jumla ya mapambano 31 ameshinda 30, sare pambano moja hajapoteza hata moja huku akiwa ameshinda kwa KO kwenye mapambano 21, AJ ameshinda mapambano 24 na amepigwa kwenye pambano moja kati ya mapambano 25 aliyopigana, lakini pia ameshinda kwa KO kwenye mapambano 22.