(Nahodha msaidizi wa Simba katika michezo miwili iliyopita, mlinzi wa kulia Shomari Kapombe akijaribu kumita mshambuliaji wa Biashara United, Denis Nkane kwenye mchezo TPL uliomalizika kwa sare 1-1 Septemba 28, 2021)
Kulekea kwenye mchezo huo utakaochezwa kwenye dimba la Jamhuri Jijini Dodoma, wachezaji watakaokosekana na ni nahodha msaidizi na mlinzi wake wa kulia tegemezi, Shomari Kapombe anayesumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu mpaka kushindwa kumalizia mchezo uliopita dhidi ya Biashara United Mara.
Simba itawakosa mlinda mlango wake mpya Jeremia Kisubi, kiungo Ibrahim Ajib, mlinzi wa kushoto Gadiel Micheal ambao sababu zao hazijawekwa wazi lakini Winga Bernard Morrison anaendelea kutumikia adhabu ya kukosa michezo mitatu baada ya kufanya kitendo ambacho si chakimaadili kwenye fainali ya FA.
Mlinzi wa kati Joash Onyango na kiungo Sadio Kanoute wawili hawa walishindwa kumaliza mchezo uliopita dhidi ya Yanga baada ya Onyango kuumia kichwani na Kanoute kuumia kwenye mguu wake.
Kwa upande wa kuzungumzia mchezo kiujumla, Matola amesema, “Tunahitaji alama tatu kwenye mchezo wa kesho kutokana na matokeo ya mechi zetu tatu za zilizopita ili kurudisha ari kikosini pamoja imani na hamasa kwa mashabiki”.
“Tunafahamu ligi ni ngumu hasa mechi za ugenini kutokana na aina za viwanja lakini tupo kamili na lengo ni moja kupata alama tatu” Matola akamaliza hivyo.
Nae kocha wa Dodoma Jiji, Mbwana Makata amesema, "Tunaiheshimu Simba na tunafahamu imetufunga katika mechi tatu zilizopita lakini hilo halitutishi. Kwenye mchezo wa leo tutacheza soka la kushambulia pamoja na kurudi kuzuia kwa pamoja tunaimani tutapata ushindi”.
Simba ipo nafasi ya 9 ikiwa na alama 1 baada ya sare ya 0-0 na Biashara United Mara ilhali Dodoma Jiji ipo nafasi ya 5 ikiwa na alama 3 baada ya kuifunga Ruvu Shooting 1-0 kwenye mchezo wa ufunguzi wa Ligi kuu.
Mchezo mwingine utakaochezwa leo ni ule utakaowakutanisha Biashara United Mara kucheza dhidi ya Ruvu Shooting saa 10:00 jioni kwenye dimba la Karume mkoani Mara.








