Jumatano , 15th Jun , 2022

Chama cha Tenisi nchini Marekani (USTA) na waandaaji wa michuano ya wazi ya Marekani (US Open) wameruhusu wachezaji wa mchezo huo kutoka mataifa ya Urusi na Belarus kushiriki katika michuano hiyo itakayofanyika kuanzia Agosti 29 mpaka Septemba 11 mwaka huu.

Wachezaji wa Urusi wameruhusiwa kushiriki michuano ya US Open

Wacheza tenisi kutoka mataifa ya Urusi na Belarus wamekuwa wakizuiwa kushiriki baadhi ya michuano ikiwemo michuano ya Wimbledon inayofanyika nchini Uingereza kuanzia Juni 27, 2022 ikiwa ni sehemu ya vikwazo kwa taifa la Urusi tangu taifa hilo lilipoivamia kijeshi taifa la Ukraine. Wachezaji hao watashiriki Lakini hawataruhusiwa kupeperusha bendera za mataifa yao watashiriki kama wachezaji huru.

Wachezaji kutoka Urusi ambao wamekutana na vikwazo ni Daniil Medvedev ambaye ni namba 1 Duniani na bingwa mtetezi wa US Open, Andrey Rublev namba 7 na mwana dada Aryana Sabalenka namba 6.

Kwa upande mwingine bingwa mara 20 wa Grandslams Novak Djokovic hatashiriki michuano ya wazi ya Marekani US Open kwa sababu hajachanja chanjo ya uviko 19. Moja ya vigezo vya kushiriki US Open ni lazima kila mchezaji kuwa amepata chanjo hiyo. Mapema mwaka huu Novak alikosa Michuano ya wazi ya Australia Australia Open kutokana na kanuni hii ya chanjo.