Alhamisi , 21st Dec , 2017

Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu ya soka ya Simba SC Zacharia Hanspoppe amethibitisha kuachana na mlinzi wake wa kati Method Mwanjali raia wa Zimbambwe.

Hanspoppe amethibitisha hilo leo huku akieleza kuwa nafasi ya Mwanjali imchukuliwa na Mghana Asante Kwasi kutoka klabu ya Lipuli FC ya Iringa.

Aidha Hanspoppe pia amesema kuwa Simba imeachana na mpango wake wa kuwasajili kiungo kutoka Zambia Jonas Sakuwaha na mshambuliaji Antonio Dayo Domingues kutoka Msumbiji.

Kwa upande mwingine Hanspoppe amemtaja winga Jamal Mnyate kuwa amejiunga na Lipuli FC kwa mkopo. Awali kulikuwa na tetesi kuwa Simba ingewaacha wachezaji wa kimataifa Mghana Nicholas Gyan na Mrundi Laudit Mavugo.

Naye beki wa kati wa Simba, Salim Mbonde anatarajiwa kuanza mazoezi Jumatatu baada ya kupona maumivu ya goti yaliyomuweka nje tangu Oktoba 15, alipoumia kwenye mechi dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Uhuru.