Jumapili , 20th Jun , 2021

Mawakala wa Mlinzi wa Real Madrid Raphael Varane wanatarajia kufungua mazungumzo na Klabu ya Manchester United mapema wiki hii baada ya mlinzi huyo kukataa mkataba mpya na Real Madrid.

Raphael Varane kushoto na Ole Gunnar Solskjaer kulia

Varane alikataa ofa ya Real Madrid ya kuongeza miaka miwili katika mkataba wake, ambao umebakiza miezi 12 kumalizika, na sasa yuko mbioni kuondoka Santiago Bernabeu baada ya kudumu kwa miaka 10 na miamba hiyo ya La Liga.

Kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer ni moja wapo ya timu kubwa zinazopenda kumsajili mchezaji huyo mwenye miaka 28 katika majira haya ya joto.