
Mlinzi wa Azam FC, Serge Pascal Wawa.
Tangu kuanza kwa michuano ya Ligi Kuu Bara msimu huu, timu hiyo iliwakosa mabeki wake wa kutumainiwa, ambao walikuwa wakisumbuliwa na majeraha kwa muda mrefu.
Kocha Mkuu wa timu hiyo Mhispania, Zeben Hernandez amesema, kurejea uwanjani kwa wachezaji hao ni habari nzuri kwake kwani ile hofu aliyokuwa nayo sasa imeondoka na anatarajia makubwa katika mechi zijazo za timu hiyo.
“Nimevutiwa na uwezo wao waliounesha katika mechi ya kirafiki, hivyo kuanzia sasa naweza kuanza kuwatumia katika mechi zetu zijazo, kwani kutokuwepo kwao katika kikosi changu, lilikuwa ni pengo kubwa sana,” amesema Harnandez.
Azam hivi sasa inashika nafasi ya saba katika msimamo wa Ligi Kuu, ikiwa na pointi 11 baada ya kucheza mechi saba na kufanikiwa kushinda tatu, sare mbili huku ikifungwa pia mechi mbili.