Alhamisi , 10th Aug , 2017

Manahodha wa timu zitakazoshiriki fainali ya michuano ya Sprite BBall Kings katika nyakati tofauti wamewasihi wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Makongo wafanye michezo na kuzingatia elimu ili ije iwasaidie katika maisha yao.

Watangazi wa EATV katika kipindi cha 5selekt Tbway, FNL Sammisago pamoja na manahodha wa timu za zilizoingia fainali ya #SpriteBBallKingsFinals2017 wakiwa pamoja na wanafunzi wa sekondari ya Makongo.

Akizungumza Nahodha wa Mchenga BBall Stars Mohamed Yusuph 'Muddy' wakati akitoa hamasa kwa wanafunzi hao amesema kupitia michezo hasa mpira wa kikapu kumeweza kumsaidia yeye kupata udhamini wa elimu na kuenda nje ya nchi kujiendeleza kupita mpira.

"Elimu na michezo ni vitu viwili vinavyoenda kwa wakati mmoja kwa hiyo ukiwa mzuri mazoezi ni lazima uwe utakuwa vizuri darasani kwa kuwa kila unachokifanya katika mazoezi unakuwa unachangamsha akili yako na kuwa mwepesi kwenye kufikilia. Tatizo kubwa lililopo kwa wanafunzi ni kwamba hatuzingatia masomo ya darasani tunaelemea sehemu moja tu", alisema Muddy.

Manahodha wa timu shiriki katika fainali za Sprite BBall Kings waliyovalia flana nyeupe wakikabidhi zawadi kwa viongozi wa serikali ya Wanafunzi Makango.

Naye nahodha kutoka timu ya TMT, Isihaka Masoud ambaye pia alisoma katika shule hiyo kidato cha tano na sita kipindi cha nyuma kidogo amewataka wanafunzi hao wajitokeze kwa wingi kuangalia fainali hizo za aina yake zitakazofanyika siku ya Jumapili katika uwanja wa Don Bosco Oysterbay Jijini Dar es Salaam.