Alhamisi , 14th Aug , 2014

Awataka vijana kutumia fulsa ndogo zilizopo kujiendeleza kimichezo badala ya kusubiri kusukumwa na mtu kwani michezo sasa ni ajira nzuri na ina pesa kuliko hata kazi za kawaida ambazo vijana wengi wanapenda kuzikimbilia

Muogeleaji Magdalena Mushi kushoto akiwa na mwogeleaji mwenzake wa Tanzania Ammaar Ghadiyali na kocha wao Sheha Mohammed.

Wanamichezo wa michezo mbalimbali wametakiwa kuwa wavumilivu,na kuwa na nidhamu,pamoja na kufanya mazoezi kwa nguvu na bidii bila kukata tama kama wanataka kufanikiwa katika mchezo ambao wanacheza

Wito huo umetolewa na mwogeleaji chipukizi wa Tanzania ambaye anasoma na kucheza mchezo huo nchini Australia Magdalena Mushi ambaye amewataka wanamichezo chipukizi kupenda kujifunza na kuzingatia mafunzo ya walimu wao wa michezo

Aidha Magdalena amewataka wazazi kuwaunga mkono watoto wao katika michezo wanayoshiriki ili kuwapa moyo wachezaji, akitolea mfano yeye mwenyewe baada ya kujifunza kupitia Nyambui na kuweza kuwika katika michezo ya kimataifa ikiwemo Olimpiki

Akimalizia Magdalena amesema wanamichezo wengi chipukizi wanakatishwa tamaa nakushindwa kujiendeleza katika medani ya michezo kutokana na ukata hasa ukosefu wa vifaa na kubwa zaidi ni ubovu ama uchakavu wa miundombinu ya kuchezea mchezo husika ama kutokuwepo kwa viwanja ama eneo la kuchezea mchezo husika

Magdalena ametolea mfano katika mambo ambayo wadau, makampuni na serikali inatakiwa kuyaangalia ni kuwekeza katika mchezo wa kuogelea kwa kujenga mabwawa mengi ya kuogelea sehemu mbalimbali hasa mashuleni kama ilivyo kwa viwanja vya michezo mingine kama soka n.k na pia kuhakikisha kunakuwepo na mashindano ya mchezo wa kuogelea katika mashule na hatimaye kuingiza katika mashindano makubwa ya ndani kama vile UMITASHUMTA, UMISETA na mengineyo ambayo baadaye yatasaidia kupata wachezaji nyota watakaoiwakilisha nchi kimataifa hapo baadaye.