Jumatano , 23rd Sep , 2020

Klabu ya Wolverhampton Wanderers ya England imekamilisha usajili wa beki wa kulia Nelson Semedo kuoka FC Barcelona ya Hisapnia na kasaini mkataba wa miaka mitatu.

Usajili wa Semedo unakifanya kikosi cha Wolverhampton Wanderers kuwa na wachezaji 9 wa kireno kwenye kikosi hicho

Semedo amejiunga kwa ada ya uhamisho inayoripotiwa kuwa ni pauni milion 32 ambayo ni zaidi ya bilion 94 kwa pesa za kitanzania na amesaini mkataba wa miaka mitatu ambao unakipengele cha kuongeza miaka miwili. Mlinzi huyo wa kimataifa wa Ureno amejiunga na Wolves kuja kuziba nafasi iliyoachwa na Matt Doherty aliyejiunga na Tottenham.

Baada ya kukamilika kwa usajili wa Semedo kikosi cha Wolves kimefikisha idadi ya wachezaji kumi wa kireno katika kikosi hicho kinachonolewa na kocha Nunu Espirito Santo ambaye pia ni mreno, wachezaji wengine wa kireno wanoaunda kikosi hicho ni Joao Moutinho, Ruben Neves, Ruben Vinagre, Rui Patricio, Vitinha, Pedro Neto, Fabio Silva, Roderick Miranda na Daniel Podence.

Beki huyo wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 26 ameitumikia FC Barcelona kwa miaka mitatu alijiunga na klabu hiyo mwaka 2017 akitokea Benifica ya nyumbani kwao Ureno, na ameitumikia Barcelona katika michezo 124 na amefunga mabao mawili huku akishinda jumla ya mataji manne ukiwemo ubingwa wa ligi kuu Hispania La Liga mara mbili.

Mlinzi huyu ameishukuru FC Barcelona kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kumuamini na kumpa nafasi muda wote aliokuwepo katika klabu hiyo.

Semedo ameandika “Asante sana Barcelona kwa kunipa ndoto ya kuvaa jezi hii. Na Asante kwa kunifanya nikue kama mchezaji na kama mtu''

Wachezaji wanaotajwa kuziba nafasi ya mlinzi huyo ndani ya kikosi cha Barcelona ni Hector Bellerin wa Arsenal, Max Aarons wa Norwich City na Sergino Dest wa Ajax.