Jumanne , 21st Mei , 2019

Golden State Warriors wamefanikiwa kuingia fainali ya NBA 2019 kwa mara ya tano mfululizo, baada ya kushinda kwa Sweep dhidi ya Trail Blazers kwenye fainali za kanda ya  magharibi.

Golden State Warriors.

Warriors sasa wamekuwa timu ya pili kufanya hivyo tangu Boston Celtic walipofanya hivyo miaka ya 1960.

Katika mchezo wa leo ambao ulikuwa wa 4  wamefanikiwa kushinda kwa vikapu 119 dhidi ya 117 katika game iliyokwenda 'over time'
hivyo kukamirisha 'Sweep' kwa Portland.

Steph Curry pamoja na Draymond Green wote walipata 'triple double'
Green akifunga pointi 18, Rebound 14 na Assists 11.

Curry amefunga pointi 37, Assists 11 na Rebound 13.

Kwa upande wa Portland 
Leonard amefunga pointi 30 na Damian Lillard pointi 28.
 
Kwa matokeo hayo Warriors wanasubiri mshindi wa kanda ya mashariki kati ya Miluweke Bucks dhidi ya Toronto Raptors.

Endapo Warriors watashinda ubingwa itakuwa timu ya pili kushinda mara tatu mfululizo tangu Lakers walipofanya hivyo miaka ya 2000.

Wameshinda

116 - 94
114 - 111
110 - 99
119 - 117