(Juu kulia, Clatous Chama, Chini kushoto Bernard Morrison na Chris Mugalu)
Kuelekea kwenye mchezo utakaochezwa kwenye dimba la Benjamin William Mkapa majira ya saa 10:00 Jioni, Simba SC inataraji kuwakosa nyota wake kadhaa kwasababu mbalimbali.
Wachezaji hao ni kiungo wake, Clatous Chama ambaye inaelezwa kikanuni hawezi kucheza michuano hiyo kwasababu alishaorodheshwa kwenye klabu ya RS Berkane alitoka huku Bernard Morrison akiwa amesimamishwa tokea Februari 4, 2022.Mshambuliaji Chris Mugalu amevunjika mkono wake, winga Kibu Denis na kiung mkabaji Taddeo Lwanga wameendelea kufanya mazoezi mepesi licha ya ukweli kwamba hawajapona vizuri majeraha waliyonayo.

