Jumatano , 19th Jul , 2017

Ikiwa zimebakia siku mbili vumbi kutimuka katika michuano ya mpira wa kikapu ya Sprite BBall Kings hatua ya nusu fainali mpaka sasa ni wachezaji watano pekee kutoka timu tofauti wanaogombea nafasi ya mchezaji bora 'MVP'.

Wachezaji kutoka timu tofauti.

Wachezaji hao ni Yassin Choma kutokea timu ya Kurasini Heat pointi 94, Baraka Mopele kutokea Flying Dribblers pointi 57,Farhan Simba akiwa na pointi 47 kutoka Mchenga BBall Stars huku Mohamed Yusuph kutoka Mchenga BBall Stars akiwa pointi 48 sawa na mchezaji wa Dream Cheaser Jovin Charles ambaye timu yake imeshatolewa katika hatua ya robo fainali, ambapo atakaye bahatika kushinda nafasi hiyo ataweza kuondoka na shilingi milioni mbili.

Pamoja na hayo, sifa moja wapo ya kuweza kushinda 'MVP' ni lazima mchezaji awe anatoka katika timu iliyoweza kushinda fainali za michuano ya Sprite BBall Kings kwa maana ya kwamba aoneshe usaidizi wake katika timu.

Kwa upande mwingine, mshindi wa kwanza wa mashindano hayo anatarajiwa kuondoka na kitita cha shilingi milioni 10 akifuatiwa na mshindi wa pili kupata milioni tatu.