
Beki kisiki wa zamani wa timu ya Simba na taifa stars Boniface Pawasa ambaye alikua mmoja wa makocha na wachezaji wa zamani waliounda jopo la wang’amuzi wa vipaji katika michezo ya mikoa ikiwa ni mchakato wa TFF katika mpango wa maboresho ya timu ya taifa stars amewataka watanzania kuacha kubeza mpango huo wa TFF.
Pawasa amesema kuwa awali Tanzania kulikua na mapungufu mengi ya wachezaji wa nafasi za beki na winga wa kushoto wanaotumia mguu wa kushoto ambapo utakuta beki ya kushoto inachezwa na mchezaji anayetumia mguu wa kulia kitu kinachopelekea apate wakati mgumu wa kuzuia mashambulizi lakini sasa mpango huo umekua suluhisho la tatizo hilo.
Aidha Pawasa amesema ni wakati sasa kwa watanzania kuuunga mkono mpango huo wa TFF na kutoa nafasi ili kazi ifanyike na inapobidi watoe ushauri na si kupinga ama kukwamisha mpango huo, kwani hizi ni zama za ukweli na uwazi.
