
Waziri Ummy Mwalimu
Waziri Ummy ameyabainisha hayo leo Septemba 14 wakati akitoa taarifa za uvumi wa uwepo wa ugonjwa wa Ebola nchini na kuwatoa hofu wananchi kuwa hakuna dalili za ugonjwa huo kuwepo licha ya kuripotiwa katika nchi jirani.
''Naomba niwatoe hofu wananchi, hadi sasa hakuna mgonjwa yoyote wa Ebola aliyethibitika kuwa na ugonjwa huo'', amesema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amezitaja dalili za ugonjwa wa Ebola ambazo ni homa kali, kuumwa kichwa, kutapika na kuharisha, viungo vya mwili kuuma pamoja na kutokwa damu katika matundu yote ya mwili.
Waziri Ummy ameongeza kuwa licha ya watanzania kuwa na utamaduni wa kupeana mikono ni vyema ukawekewa tahadhari ya kunawa mikono mara kwa mara.