Alhamisi , 27th Jan , 2022

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohamed Mchengerwa ameagiza kuanzwa kwa mchakato wa kupata vijana wenye vipaji kila pembe nchini ili waje kuiwakilisha timu ya Taifa siku za usoni kwenye michuano ya Kimataifa.

(Mhe. Waziri wa Michezo, Mohamed Mchengerwa na Kikosi cha Taifa Stars)

"Tunakuja na mkakati kabambe wa kutafuta vipaji kila kijiji nchini nzima. Nimeshaagiza wenzangu kwenye Wizara wajipange kweli kweli”

“Kwahiyo tutakwenda na mkakati wa kutafuta vijana wenye vipaji kwa ajili ya maandalizi ya Soka la Kimataifa. Kama litakuwa soka la Afrika, kama litakuwa soka la Dunialakini maandalizi lazime yaanze sasa" amesema Waziri Mchengerwa.

Waziri huyo wa utamaduni Sana na michezo ameyasema hayo akiwa Rufiji Mkoani Pwani wakati akizungumza na watendaji kuhusu mikakati ya Wizara hiyo katika kukuza Utamaduni, Sanaa na Michezo hapa Nchini.

Sambamba na hilo, Waziri Mchengerewa amewataka Maafisa Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhakikisha Michezo na Sanaa inazungumzwa kila mtaa kwa kuwa serikali inafedha ya kutosha kukuza sekta hiyo.