Ijumaa , 20th Jun , 2014

Klabu ya soka ya Yanga inataraji kuanza mazoezi wiki ijayo wakiwa na kikosi cha wachezaji kadhaa ambao hawana majukumu ya kuziwakilisha timu zao za taifa

Kikosi cha Dar es salaam Yanga katika moja ya michezo ya ligi kuu Tanzania bara msimu uliopita.

Kikosi kamili cha klabu ya soka ya Dar es salaam Young Africans kinatarajia kuanza mazoezi rasmi Jumatatu ya juma lijalo tayari kujiwinda na michuano ya ligi kuu msimu ujao na michuano ya kimataifa ambayo klabu hiyo itashiriki msimu huu

Afisa habari wa timu hiyo Baraka Kizuguto amesema kuwa wachezaji wote wa kikosi hicho ambao hawatakuwa kwenye timu zao za taifa ndio wataanza mazoezi hayo chini ya kocha msaidizi Boniface Mkwasa

Aidha Kizuguto amesema wanamwamini kocha Mkwasa na jopo lake la ufundi na hivyo ataendelea kusimamia na kuongoza programu za mazoezi kama kawaida mpaka pale kocha mkuu mtarajiwa Mbrazil Marcio Maximo ambaye aliwahi kukinoa kikosi cha taifa stars atakapowasili nchini nakuanza programu yake mpya ya mazoezi.