Jumapili , 9th Mar , 2014

Klabu wa Yanga itawakabili Al Ahly huku kikosi chao kikiwa hakina majeruhi.

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya klabu bingwa barani afrika, Dar Yanga Africans, baadaye leo watashuka kwenye dimba la El Max mjini Alexandria nchini Misri kuwavaa mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Al Ahly.

Yanga ambayo ilipata ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza, inahitaji ushindi au sare ya aina yoyote ili iweze kuwavua ubingwa Al Ahly ambao wanasifika kwa fitna nyingi hasa wakicheza nyumbani kitu ambacho Yanga wanakijua kwani walishaelezwa hilo mapema na Rais wa TFF, Jamal Malinzi, juu ya mbinu chafu na uchezaji wa hila wa Mashetani Wekundu hao wa Cairo.