Jumatano , 24th Jan , 2018

Baada ya TFF kufanya ukaguzi katika viwanja vya timu zinazoshiriki Kombe la Shirikisho hatimaye imezuia viwanja vitatu kutumika kwa mechi zinazofuata za hatua ya raundi ya tatu.

Shirikisho hilo la soka nchini limevitaja viwanja ambavyo havitatumika katika raundi hiyo ya tatu ni pamoja na Uwanja wa Nachingwea unaotumiwa na Majimaji Rangers ambao watalazimika kwenda Ilulu Lindi kucheza dhidi ya Mtibwa Sugar.

Uwanja mwingine ambao hautatumika ni wa CCM Mkamba Morogoro ambao hutumiwa na timu ya Shupavu, hivyo mchezo kati ya timu hiyo na Azam FC utapigwa kwenye dimba la Jamhuri Morogoro kwa mchezo wake na Azam FC.

Kwa upande wa timu ya Ihefu ya Mbarali inayokutana na Yanga haitatumia uwanja wake  wa Mbarali Estate hivyo italazimika kwenda jijini Mbeya kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine kucheza mchezo wake huo wa raundi ya tatu Kombe la FA.