Jumatatu , 13th Jun , 2022

Klabu Yanga imewataka mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Juni 15, 2022 siku ya Jumatano dhidi ya klabu ya Coastal Union ya Tanga utakaochezwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

(Afisa Msemaji wa Yanga SC, Haji Manara)

Akizungumza na Wanahabari, Afisa Msemaji wa Yanga Haji Manara amesema wachezaji wanapenda kuona mashabiki wanajitokeza kwa wingi ili kutoa hamasa kwa wachezaji ili waweze kushinda mchezo na kutangazwa kuwa mabingwa wapya msimu wa 2021/22.

"Tunawaheshimu Coastal kwa historia yao japo hawana vikombe vingi lakini Yanga sio timu ya kushindwa na wachezaji wanawahitaji mashabiki kuja kuwapa hamasa. Viingilio ni 5,000,10,000 na 15,000. Mchezo wetu kuanza saa 20:30 usiku" amesema Manara