Jumatano , 3rd Jun , 2020

Kupitia kipindi cha Kipenga Xtra, mashabiki wa Yanga na Simba wametambiana huku kila upande ukibeza uwekezaji wa upande mwingine, ambapo Yanga wanasema Simba imekwama na Simba wanabeza ushirikiano wa Yanga na La Liga.

Mashabiki wa Simba na Yanga

Wakiongea leo, katika kipindi hicho cha mashabiki kuanzia Saa 6:00 hadi Saa 7:00 mchana, mshabiki hao wameeleza mengi.

''Sisi Yanga hatuwezi kukosea wala kukwama kwenye mabadiliko yetu kama walivyokwama Simba, maana tunafuata taratibu zote na tuna watu makini ndio maana hata La Liga wamekubali kusaini na sisi kwenye hili'' - Timothy Levy, Shabiki Yanga.

Kwa upande wake shabiki wa Simba Aggy Daniel amesema, ''Watu wanamlisha maneno Mo Dewji kila akiandika kitu kuhusu kampuni wanasema Simba utadhani ana kampuni moja tu ya Simba, wakati ana makampuni mengi, me nadhani tuache kumlisha maneno''.

Naye Justine Joel wa Simba akaongeza kuwa, ''Suala la uwekezaji Simba hata ukienda miaka 10 mimi nitavumilia lakini muhimu Simba ipate ushindi tu na kwenda mbele hilo la uwekezaji tunawaachia walioko juu pale''.

Justine akamaliza kwa kusema, ''Haya mabadiliko ya Yanga yanayotajwa kuwa La Liga wanashiriki yananishangaza sana maana kwenye kusaini sikuona mwakilishi wa La Liga ila kulikuwa na Scarf za La Liga tu''.

Akijibu hoja hiyo ya Simba, shabiki wa Yanga Mohammed Mabesi akasema, ''Mimi nachojua, Yanga tutafanya kazi na La Liga kwa miaka mitatu na nusu wakitushauri kuhusu mfumo wa mabadiliko na wanachama watashiriki kuchagua sasa ni mfumo upi sahihi katika mependekezo yatakayotolewa''.
 

Zaidi Tazama Video hapo chini