Jumatano , 7th Dec , 2016

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema haina mpango wa kuachana na kocha wake msaidizi Juma Mwambusi, licha ya kupata kocha mwingine msaidizi kutoka nchini Zambia, anayeitwa Noel Mwandila

Kocha Juma Mwambusi akiwa na kikosi cha Yanga

 

Kaibu Katibu Mkuu wa Yanga Baraka Deusdedit amesema uongozi wa klabu haujafikiria kuachana na Mwambusi, na kwamba kuanzia sasa timu hiyo itakuwa chini ya makocha wasaidi wawili.

Kuwasili kwa kocha huyo msaidizi kunafanya timu hiyo hadi sasa kuwa na jumla ya makocha wanne katika nafasi tofauti ambao ni Hans van der Pluijm (Mkurugenzi wa Ufundi), George Lwandamina (Kocha Mkuu), Juma Mwambusi (Kocha Msaidizi) na Noel Mwandila.