
Akiongea leo Juni 20, 2019 kwenye makao makuu ya klabu hiyo katibu mkuu Fredrick Mwakalebela, ameweka wazi kuwa wao kama klabu wameshaongea naye na wakampa nafasi kilichobaki ni yeye kuamua.
“Ibrahimu Ajib mkataba wake unamalizika mwisho wa mwezi huu, mazungumzo yamefanyika na klabu imempa nafasi ya kuamua kama anapenda kubaki nafasi ipo, lakini kama anataka kuondoka klabu inamtakia kila la kheri” - Mwakalebela
Aidha Yanga imetangaza kuwa Kilele cha 'Wiki ya mwananchi' kitakuwa tarehe 27/07/ 2019 kwenye uwanja wa taifa ambapo watakuwa na kauli mbiu ya ‘Funga kazi, Kusanya kijiji’
Zaidi tazama Video hapo chini.