Alhamisi , 19th Sep , 2019

Klabu ya Yanga, leo Septemba 19, 2019 imemtangaza rasmi ndugu Hassan Bumbuli kuwa Afisa Habri na mawasiliano wa klabu hiyo.

Makao Makuu ya Yanga

Taarifa hiyo iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Yanga, Dismas Ten, imesema kuwa Mwenyekiti wa klabu, Dkt. Mshindo Msolla amemteua Hassan Bumbuli kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji.

Aidha katika hatua nyingine, Dkt. Msolla pamoja na Kamati ya Utendaji wamemtangaza rasmi ndugu Antonio Nugaz kuwa Afisa Mhamasishaji wa klabu hiyo.

Soma taarifa rasmi ya klabu hapa chini.