Jumatatu , 11th Nov , 2019

Klabu ya soka ya Yanga leo Novemba 11, 2019, imetangaza uteuzi wa Katibu Mkuu mpya, ambaye anakuwa mtendaji mkuu wa klabu hiyo.

Makao makuu ya Yanga mitaa ya Jangwani Dar es salaam.

Taarifa ya Yanga imemtaja David M. Ruhago kuwa ndio Katibu Mkuu, ambaye ameteuliwa na Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo chini ya Mwenyekiti wake Dkt. Mshindo Msolla.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa uteuzi huo unaongeza idadi ya watendaji ndani ya klabu hiyo.

Ruhago amekuwa mjumbe wa kamati mbalimbali za klabu hiyo katika vipindi tofauti tofauti.