Yanga yathibitisha safari yake

Jumatatu , 12th Feb , 2018

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga SC imethibitisha kuwa tayari mipango kwaajili ya safari yake kuelekea Shelisheli kwenye mechi ya marudiano dhidi ya St. Louis yamekamilika na timu hiyo inatarajiwa kuondoka nchini Jumapili.

Jumapili itakuwa ni Februari 18 ambapo itafika nchini humo siku hiyohiyo na kuanza maandalizi kwa mchezo huo utakaopigwa Jumatano Februari 21 kwenye uwanja wa Stadelinite mjini Victoria.

Katika mchezo huo wa klabu bingwa Africa, Yanga inaongoza kwa bao 1-0 kufuatia ushindi ilioupata kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam siku ya Jumamosi hivyo inahitaji ushindi au sare ya aina yoyote ili kusonga mbele.

Kabla ya mchezo huo Yanga itacheza mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara dhidi ya Majimaji FC kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam siku ya Jumatano.

''Kikosi cha @yangasc1935 kinatarajia kuondoka nchini jumapili asubuhi kuelekea Shelisheli tayari kwa mchezo wa marejeano na @stloiusfc kwenye uwanja wa #stadelinite feb 21. #cafchampionsleague'', wameandika Yanga kupitia Ukurasa wao wa Twitter.