Jumatatu , 20th Jul , 2020

Kama unaweza sema ligi imemalizika kwa kuwa bingwa wa VPL ameshapatikana, basi ligi hiyo bado ina mechi nzuri na za ushindani, kutoka kwa timu zinazogombea kujinasua kushuka daraja.

Alliance ni moja ya timu zilizopo nafasi ya kushuka daraja

Kama unaweza sema ligi imemalizika kwa kuwa bingwa wa VPL ameshapatikana, basi ligi hiyo bado ina mechi nzuri na za ushindani, kutoka kwa timu zinazogombea kujinasua kushuka daraja.

Kuanzaia nafasi ya 15 na 16 ambazo ni nafasi za Lipuli na Mwadui kila mmoja anapambana kutoka kwenye nafasi hizo ambapo ni kwenda kucheza mtoano (play off) lakini pia wanaweza kushinda ili wasishuke daraja kwa sababu timu za Ndanda, Alliance na Mbao zinanyemelea nafasi hizo za kucheza play off.

Lakini kibarua kigumu kipo kwa Mbeya City walio nafasi ya 13 na Mtibwa Sugar nafasi ya 14 ambao wapo hatarini kusogea eneo la kushuka daraja kutokana na ugumu wa mechi zao.

Mbeya City inakutana na Azam fc Chamazi, wakati Mtibwa Sugar inakutana na Yanga, Mogorogo Julai 22.

Mechi hizi zinakuwa ngumu kwao kwa sababu Azam fc, Yanga na Namungo wanagombea nafasi ya pili kila mmoja.

Mechi nyingine itakayokuwa na burudani ya aina yake ni Alliance na Ndanda ambao wote wapo eneo la kushuka daraja lakini ushindi wa mechi zao mbili kila mmoja anaweza kunusurika kubaki ligi kuu.

Kuanzia nafasi ya 15 na 16 ambazo ni nafasi za Lipuli na Mwadui kila mmoja atapambana kutoka kwenye nafasi hizo ambapo ni kwenda kucheza mtoano (play off).

Lakini salama ya timu hizo ni kushinda tu, ili wasishuke daraja kwa sababu timu za Ndanda, Alliance na Mbao wananyemelea nafasi hizo za kucheza mtoano (play off).

Lakini kibarua kigumu kipo kwa Mbeya City walio nafasi ya 12 na Mtibwa Sugar nafasi ya 13 ambao wapo hatarini kusogea chini kutokana na ugumu wa mechi zao.

Mbeya City anakutana na Azam fc Chamazi, wakati Mtibwa Sugar anakutana na Yanga, Mogorogo.

Mechi mbili zilizobaki kwa kila timu za ligi kuu ya VPL zinaweza kuitoa timu kwenye eneo salama hadi kushuka daraja au kushuka daraja hadi eneo salama, kutokana na timu kutofautiana alama chache sana.
Ikiwa tayari Singida United imeshashuka daraja, timu za Alliance, Mbao na Ndanda zinasubiri pumzi ya mwisho kuungana na Singida.