Jumapili , 19th Mei , 2019

Kocha mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amekabidhiwa majukumu ya kuziongoza timu zote za klabu hiyo kuanzia sasa.

Mwinyi Zahera

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Dr. Mbette Mshindo Msolla kwenye hafla maalumu ya Iftar iliyoandaliwa na uongozi wa klabu pamoja na kamati ya kuhamasisha michango ya klabu, ambayo imefanyika jana jijini Dar es salaam.

Dr. Msolla amesema, "kwa sababu ya masuala ya ufundi, timu zote zitakuwa chini ya kocha Mwinyi Zahera. Ni lazima kama timu tuwe na filosofia ya klabu yetu kwahiyo kwenye timu zote za vijana na Yanga Princess lazime falsafa za Zahera zitumike".

Pia Dr. Msolla ameongeza kwa kuwataka wana Yanga kuwa na umoja na kusisitiza kuwa katika ahadi zake kipindi cha kampeni ni kuleta umoja na kuileta klabu karibu na wanachama. 

Suala lingine ni kubadilisha mfumo wa kiuendeshaji wa klabu, ambapo amesema kuwa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja atahakikisha Yanga inaenda katika mabadiliko ya mfumo ambao tayari ulishapitishwa na wanachama.

Msikilize hapa Dr. Mbette Msolla akielezea zaidi utekelezaji wa ahadi zake kwa wanachama.