Jumanne , 30th Jul , 2019

Kocha Mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa usajili wa klabu hiyo umekamilika kwa asilimia kubwa na malengo yametimia kuelekea msimu mpya wa 2019/20.

Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera

Akizungumza ikiwa ni siku ya pili tangu aliporejea kambini Yanga, kocha Zahera amesema kuwa sasa amebakiza mchezaji mmoja pekee ambaye akishawasili watakuwa wamekamilisha rasmi usajili.

"Malengo tuliyokuwa tumeweka kwenye usajili yametimia, amebaki mchezaji mmoja (mshambuliaji) alipaswa kuingia juzi nadhani ataingia leo", amesema Zahera.

"Akifika huyo striker mambo yote ya usajili yatakuwa sawa", ameongeza.

Klabu ya Yanga ipo katika 'wiki ya Wananchi' iliyozinduliwa hivi karibuni ikiwa na lengo la kuhamasisha wanachama na mashabiki katika kufanya shughuli mbalimbali za kijamii mpaka siku ya kilele chake, Agosti 4 ambapo itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Kariobangi Sharks ya Kenya.