Jumatatu , 21st Mei , 2018

Kwenye imani ya dini zote duniani kuna Amri 10 za Mungu ambazo wote ulimwenguni tunazifuata, lakini hii imekuwa kinyume kwa wafuasi wa dini ya Iglesia Maradoniana, ambayo asili yake ni huko Argentina.

Dini ya Iglesia Maradoniana ilianzishwa mwaka 1998 na wafuasi wa mcheza soka maarufu duniani na mzaliwa wa Argentina, Diego Maradona ambapo wafuasi hao wanamsujudu Maradona kama Mungu wao.

Kwenye dini hiyo ambayo mpaka sasa ina wafuasi takriban laki 2 mpaka sasa, Amri zao 10 sio zile ambazo wengi tunazifahamu, wao wana amri zao 10 ambazo ukiwa mfuasi ni lazima uzifuate kwama zilivyo kwa Amri 10 za Mungu, nazo ni :

1.Mpira haujawahi kuchafuliwa

2. Penda soka zaidi ya yote

3. Tangaza mapenzi ya dhati kwa Diego Maradona na uzuri wa soka

4. Tetea jezi ya Argentina

5. Sambaza habari za Diego Maradona na miujiza yake ulimwenguni pote

6. Enzi hekalu alilochezea na mashati yake matakatifu

7. Usimtangaze Diego kama mwanachama wa timu yoyote.

8. Hubiri na kueneza kanuni za Kanisa la Maradona.

9. Lifanye Diego kuwa jina lako la kati kati

10. Mpe mtoto wako wa kwanza wa kiume jina la Diego

Dini hiyo haijaishia hapo tu, kwani pia ina sala yake maalum kama ambavyo Wakristo wana sala ya Bwana (Ba ba Yetu) ambayo wao wanaita Diego wetu (Our Dieo), inayomuomba Diego Maradona ikisema ..'Diego wetu,uliye dimbani, mguu wako wa kushoto utakaswe, tuletee uchawi wako, fanya magoli yakumbukwe mbinguni na duniani, tupatie uchawi kila siku, samehe kikosi cha Uingereza, kama tulivyowasamehe Napolitan Mafia, usiruhusu kukamatwa nje, na utuokoe kutoka kwa Havelange na Pele.

Nikikufafanulia zaidi baadhi ya watu waliotajwa kwenye sala hiyo ya 'Our Diego' ni hawa

Napolitan Mafia ni kundi la kimafia lililokuwa likijihusisha na uuzaji wa madawa ya kulevya, ngono na baadhi ya mambo yasiyofaa ya uvunjaji sheria.

Havelange alikuwa ni mwanasheria wa Brazil ambaye alikuwa Rais wa FIFA mwaka 1974- 1998) .

Pele ni mcheza soka maarufu duniani kutoka Brazil.

Wafuasi wa Igresia Maradoniana
Diego Maradona mwenyewe