Zitto aguswa na hali ya Samatta

Jumanne , 13th Feb , 2018

Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amemtembelea nahodha wa Taifa Stars anayecheza soka la kulipwa KRC Genk nchini Ubelgiji, Mbwana Samatta na kudai amefurahi kumkuta mzima.

Zitto ameeleza hayo muda mchache alipokutana na mchezaji huyo nyumbani kwake huko Ubelgiji ambapo Mbunge huyo alienda kwa ajili ya shughuli maalumu za chama chake. 

"Nimefurahi kupita kumsalimu na kumjua hali Samatta, nimefurahi zaidi kumkuta akiwa ni mzima wa afya na anashiriki mazoezi ya timu yake bila shida. Inatia moyo zaidi kuona kijana huyu mwenzetu wa kitanzania namna anavyofanya kazi kwa bidii ili aweze kufanikiwa zaidi", amesema Zitto.

                                      Zitto akiwa katika picha ya pamoja na Samatta.

Kwa upande mwingine, Zitto amemuomba dua mchezaji huyo wa kimataifa aweze kutimiza ndoto zake alizokuwa nazo maishani mwake.