Masogange afariki dunia

Ijumaa , 20th Apr , 2018

Mwanamitindo na video queen marufu bongo Agnes Gerald maarufu kama Masogange, amefariki dunia jioni ya leo April 20 alipokuwa amelazwa katika hospital ya Mama Ngoma akipatiwa matibabu

Akithibitisha taarifa ya kifo hicho Daktari Rama Ngoma wa hospitali ya Mama Ngoma, amesema Agnes amefariki dunia kwa tatizo la pneumonia na upungufu wa damu jioni hii, na alikuwa amelazwa hospitalini hapo kwa muda wa siku nne mpaka kifo kilipomkuta.

Tayari mwili wake umeshatolewa hospitali ya Mama Ngoma, na kwa mujibu wa muigizaji Steve Nyerere umepelekwa hospitali ya Taifa ya muhimbili.

Agnes Masogange alikuwa maarufu baada ya kuonekana kwenye video kadhaa za bongo ikiwemo Masogange ya Belle 9.