Jumatatu , 10th Aug , 2015

Baraza kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi CUF, Taifa kwa niaba ya Mkutano Mkuu limeunda kamati ya watu watatu watakaofanya kazi zilizoachwa na aliekua mwenyekiti wa chama hicho Pro. Ibrahimu Lipumba.

Kaimu Naibu katibu mkuu wa CUF, Zanzibar Ismail Jussa Ladhu

Akizungumza jana Kaimu Naibu katibu mkuu wa CUF, Zanzibar Ismail Jussa Ladhu amesema kuwa kamati hiyo imeundwa kwa mujibu kwa wa katiba ya CUF na kuongeza kuwa kamati hiyo itafanya kazi kwa muda wa miezi sita mpaka mkutano mkuu mwengine wa chama hicho utakapoitishwa.

Amesema kuwa kamati hiyo ambayo itafanya kazi hadi uchaguzi mkuu ili kukivusha chama hicho hadi uchaguzi mkuu imewateua wanasiasa wazoefu ili kuweza kufanua kazi hiyo kwa ufanisi zaidi.

Aliwataja wanaounda Kamati hiyo ni pamoja na Twaha Issa Taslima ambae ni Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Abubakari Khamisi Bakari ambae ni Waziri wa Sheria wa Zanzibar na Severina Mwajage ambae ni makamu mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake CUF.

Aidha Jusa amekiri kuwa kuondokewa na kiongozi walimzeoa kwa muda mrefu ni pengo lakini chama kimejidhatiti vya kutosha na kusimamia misamo yake ya kutaka kukitoa Chama cha Mapinduzi Madarakani wakiwa na Umoja huo.