
Katika taarifa yake, Kaimu katibu mkuu wa Shirikisho la Riadha nchini RT Ombeni Zavalla amesema, wanariadha waliokata tiketi ya kushiriki mashindano hayo ni Ismail Juma, Ezekiel Ngimba, Fabian Joseph na Bazil Baynit ambapo wataondoka mapema ili kuwez kupata kuda wa kutosha wa kupumzika kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.
Zavalla amesema, wanariadha hao wataongozana na kocha wao Francis John ambapo wanaamini wataipeperusha vizuri bendera ya nchi katika michuano hiyo.