
Mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati, walianza kupata bao kupitia kwa Singano ‘Messi’ kabla ya Bakari Kigodeko kuisawazishia Mwadui FC ya kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.
Hilo linakuwa bao la tatu kwa Azam FC kufungwa ndani ya mechi 15 ilizocheza tangu kurejea kwa kocha Muingereza, Stewart Hall Juni mwaka huu ambapo awali ya hapo, ni Friends Rangers pekee walioweza kuupenya ukuta wa Azam FC na kufunga mara mbili wakilala 4-2 katika mchezo wake wa kwanza kabisa wa kirafiki.
Baada ya hapo, Azam FC ilishinda 1-0 dhidi ya JKT Ruvu Chamazi, 1-0 dhidi ya African Sports Tanga, 1-0 dhidi ya Coastal Union Tanga, zote zikiwa mechi za kirafiki kabla ya kuingia Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame na kushinda mechi zote hadi kutwaa ubingwa.