Jumatatu , 25th Jan , 2016

Mwingereza Johanna Konta anaweza kuandika historia ya kuwa mcheza tenesi wa kwanza Mwingereza toka mwaka 1984 kutinga hatua ya nusu fainali ya Grand Slam katika michuano ya wazi ya Australia .

Nyota huyu anayeshika nafasi ya 47 kwa ubora wa viwango duniani atashuka dimbani leo hii kuchuana na Ekaterina Makarova.

Konta mwenye umri wa miaka 24 atakuwa na kibarua kizito kuweza kuandika historia mpya ambayo waingereza wengi wanaitegemea kutoka kwake.

Mwaka 1984, Mwingereza Jo Durie, alifika hatua ya nane bora katika michuano ya wazi ya Wimbledon' na hakuna mchezaji wa tenesi wa kike wa Uingerza amewahi kufika hatua hiyo ya nane bora.

katika mchezo mwingine mwanadada Victoria Azarenka ataumana na Mjerumani Angelique Kerber katika mchezo mwingine wa robo fainali wa michuao hiyo.