
Mwenyekiti Tume ya Uchaguzi nchini NEC Jaji Damian Lubuva katikati,kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC Emanuel Kawishe na kushoto Mkuu wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga kura wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Giveness Aswile.Mapema leo wakati wakizungumza na waandishi wa Habari
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imemteua Mhe. Ritha Kabati, Mhe. Oliver Semuguruka, wa Chama cha Mapinduzi (CCM), na Mhe. Lucy Fidelis Owenya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kuwa wabunge wa viti maalumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Uteuzi huo umekuja baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa majimbo nane ambayo yaliahirishwa kwa sababu tofauti katika uchaguzi Mkuu wa tarehe 25 Oktoba mwaka jana ambapo zilibakia nafasi 3 baada ya uteuzi wa awali kuwachagua wabunge 110 kati ya 113 waliopaswa kuteuliwa kisheria.
Mwenyekiti wa NEC Jaji Mstaafu Damian Lubuva amesema kuwa uteuzi wa awali ulihusisha vyama vilivyofikisha asilimia 5 ya kura zote za wabunge kama matakwa ya Katiba yanavyotaka.
