Baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Kilakala ya wasichana wa vipaji maalumu iliyipo mkoani Morogoro
Wakizungumza shuleni hapo baadhi ya wanafunzi hao wamesema tangu serikali ilipo tangaza kutoa elimu bure wazazi wamekuwa hawawapi mahitaji muhimu huku wakilalamikia uchakavu wa miundombinu ya shule ambapo wameomba wazazi kuunga mkono jitihada za serikali ili waweze kusoma kwa utulivu na kufaulu katika masomo yao.
Kufuatia changamoto hizo wanafunzi waliosoma katika shule hiyo mwaka 1993 wamejitokeza kusaidia kupunguza baadhi ya changamoto hizo kwa kutoa vifaa vya kupakulia chakula madishi zaidi ya 80 yenye thamani ya shilingi milioni mbili na kueleza shule hiyo imesomesha viongozi wakubwa wa serikali .
Kwa upande wao baadhi ya wazazi wameleza kusikitishwa kwao na wazazi wenye tabia ya aina hiyo kuacha kwani serikali imeamua kutoa elimu bure kwa wanafunzi ili kuwapunguzia mzigo wazazi pamoja na walezi ambapo wangetumia fursa hiyo kuwatimizia wanafunzi mahitaji yote kitendo ambacho kingeweza kuwasaidia kusoma kwa bidii na kufaulu mitihani.






