
Mtoto wa kike mmoja mwenye umri chini ya miaka 15 huolewa kila baada ya sekunde saba duniani, kwa mujibu wa ripoti mpya ya Shirika la Save the Children.
Utafiti wao unaonyesha watoto wa kike wenye umri hadi wa miaka 10, hulazimishwa kuolewa na wanaume wenye umri mkubwa katika mataifa ya Afghanistan, Yemen, India na Somalia.
Machafuko, umasikini na migogoro ya kibinadamu inaonekana kuwa ni sababu kuu zinazochangia mtoto wa kike kutumbukia kwenye ndoa za utotoni.
Watoto wa kike wanaoolewa mapema hushindwa kuendelea na shule, na hujiweka kwenye uwezekano kufanyiwa ukatili, kudhalilishwa na kubakwa.