Jumatano , 12th Oct , 2016

Waalimu sita wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Njombe baada ya kudaiwa kumshambulia mwanafunzi wa kike wa kidato cha nne kwa kosa la kukutwa simu ya mkononi katika begi lake la chuma la nguo na waalimu wake.

Dkt. Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi

Tukio hilo limetokea ikiwa ni siku chache baada ya kutokea kwa tukio la kushambuliwa mwanafunzi wa shule ya sekondari ya kutwa ya Mbeya ikiwa ni adhabu aliyopewa na walimu wake waliokuwa katika mafunzo kwa vitendo shuleni hapo.

Mwanafunzi huyo wa shule ya binafsi ya sekondari ya Mbogamo, ya mkoani Njombe, Elizabeth Simfukwe anadaiwa kushambuliwa na mkuu wa shule akiwa na waalimu wengine na kumsababishia maumivu kisha kulazwa katika Hospitali ya Kibena mkoani Njombe kwa siku zaidi ya tatu akipatiwa matibabu akiuguzwa na mzazi wake anayetokea mkoa wa Songwe.

Baada ya mwandishi wa habari kufika katika Hospitali ya kibena ya mkoani Njombe ambapo mwanafunzi huyo amelazwa, Uongozi wa Hospital hiyo umesema kuwa umezuiliwa kuzungumzia taarifa hiyo kutokana na suala hilo lipo chini ya vyombo vya usalama.

Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri akiongea na East Afrika Radio kwa njia ya simu amekiri kutokea kwa tukio hilo wilayani kwake licha ya yeye kuwa mbali ofisi amesema ni kweli mwanafunzi huyo alikutwa na kosa lakini sheria iliyotumika kumuadhibu ni kinyume cha sheria zilizowekwa na serikali.

Kituo hiki kilifika shuleni hapo na kubaini kutokuwepo kwa walimu hao na kuthibitika kuwa wanashikiliwa na vyombo vya usalama huku shule hiyoi ikiwabakiwa na mwalimu mmoja tu kutokana na tukio hilo.

Baadhi ya viongozi waliofika hospitalini hapo na kuzungumza na mwanafunzi huyo wameeleza hali yake huku baba wa mtoto huyo anakili mwanaye kupigwa, huku shuleni kukiwa hakuna walimu. Sauti za Baadhi ya viongozi pamoja na baba Mzazi wa mwanafunzi huyo na mwanafunzi mwenyewe. 1. Mhe. GEORGE SANGA DIWANI RAMADHANI 2. Mhe. ABUU MTAMIKE, DIWANI MJI MWEMA 3. SIMFUKWE BABA WA MTOTO 4. MWANAFUNZI
Sauti ya Kaimu Mganga Mfawidhi DR. SELINA NYONI, MGANGA MFAWIDHI
ANTON MTWEVE KAIMU AFISA ELIMU HALMASHAURI, aliyedai kuwa hakuwa na taarifa
RUTH MSAFIRI MKUU WA WILAYA NJOMBE