Jumatano , 12th Oct , 2016

Bondia Thomas Mashali anaweza kushuka ulingoni mwishoni mwa mwaka huu, kuzichapa na bondia wa Malawi Chimwemwe Chiwotcha, kutetea ubingwa wa dunia, ikiwa mipango hiyo itakaa sawa.

Thomas Mashali

Akizungumza na East Africa Radio, Mashali amesema kwa sasa amejichimbia Bagamoyo mkoani Pwani, akifanya mazoezi makali kwa ajili ya pambano lolote litakalokuja mbele yake, akitarajia kuanza na Mmalawi katika mwezi wa Desemba mwaka huu.

Mashali, alishinda taji la dunia mkanda wa WBU, baada ya kumshinda kwa pointi bondia wa Iran, Sajad Mehrabi katika mwezi wa Mei mwaka huu, na inabidi autetee mkanda huo hivi karibuni.