
Kansela wa Ujerumani akifungua Jengo nchini Ethopia
Merkel ametaka wapinzani wapewe nafasi ya kuandamana na washirikishwe kwenye mijadala ya kidemokrasia kwa kuwa katika nchi ya kidemokrasia, kunapokuwa na upinzani, kuna haja ya kuwa na uhuru wa vyombo vya habari.
Bi. Merkel amesema ni jambo la kawaida kwa watu kutaka kuelezea maoni yao katika nchi ambayo imepambana na umaskini kwa kiasi fulani na watu wake wameelimika.
Katika hatua nyingine Kansela Markel amesema Ujerumani imejitolea kuwapatia mafunzo polisi wa Ethiopia kuhusu namna ya kutuliza ghasia panapokuwa na maandamano.
Ziara hii ya Kansela Merkel inafanyika siku tatu tu baada ya Ethiopia kutangaza hali ya hatari baada ya watu wasiopungua 50 kuuawa kwenye maandamano ya kuipinga serikali katika siku za hivi karibuni