Alhamisi , 13th Oct , 2016

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu, ameitaka Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) kutoa elimu kwa wananchi kuhusiana na mfumo mpya wa kielektroniki wa utoaji taarifa za madhara ya dawa.

Afisa Uhusiano TFDA, Gaudensia Simwanza

Akizungumza Jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa mfumo wa kielekitroniki wa utoaji wa taarifa za madhara ya dawa, Waziri Mwalimu amesema mfumo huo utawezesha watendaji wa afya, wagonjwa na wananchi kutoa taarifa za madhara yanayohisiwa kusababishwa na matumizi ya dawa.

Aidha waziri amewasihi TFDA kushirikiana na SIDO ambao wana dhamana ya kuendeleza viwanda vidogo vidogo kwa ajili ya kuwasaidia wajasiliamari wadogo kuhakikisha bidhaa wanazozalisha ni salama.

Naye Mkurugenzi wa TFDA, Profesa Hiti Sillo, amesema mfumo huo utakuwa ni wa kieletroniki ambao utakuwa kwenye simu na kompyuta zilizounganishwa kwenye mtandao (internet)

Aidha amesema kabla ya kuzindua mfumo huu wameweza kufanya majaribio katika mwezi Juni hadi Agosti 2016 na kuweza kupokea taarifa za madhara ya dawa zipatazo 36 na hivyo kuongeza taarifa zinazopokelewa