Alhamisi , 1st Dec , 2016

Serikali imewahakikishia wawekezaji katika sekta ya viwanda kuwa hakuna tatizo la upatikanaji wa makaa ya mawe wala uhaba wa gesi kwa ajili ya kuendesha viwanda kama inavyoenezwa.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage.

 

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage mesema watanzania hawana sababu ya kupatwa na hofu juu ya uvumi huo na kuwahakikishia kuwa serikali itaendelea kuwajali na kuwakaribisha wawekezaji wa viwanda na pia kuhakikisha wanaungwa mkono katika uwekezaji wao.

Waziri Mwijage amesema kuwa kuhusu makaa ya mawe ambayo yanazalishwa nchini kwa ajili ya viwanda ni bora na yanapatikana kwa bei rahisi tofauti na habari zinavyoenezwa kuhusu makaa hayo na kusema wanauza kwa bei hiyo kwa ajili ya kuendeleza viwanda nchini.

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.

 

Kwa upande wake Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa mwa kujibu wa takwimu Tanzania ina uwezo wa kutumia makaa ya mawe yaliyopo kwa zaidi ya miaka 200 ijayo hivyo hawana sababu ya kuyauza kwa bei ya juu kwenye viwanda nchini.