Jumatatu , 12th Dec , 2016

Shirikisho la Soka Tanzania limekiri kuwa kuna wachezaji wasio kuwa nasifa kiumri wameshiriki katika ligi ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 iliyohitishwa siku ya jana.

Mabingwa wa kwanza wa michuano ya vijana U20, Simba SC wakishangilia

Mkurugenzi wa ufundi wa TFF, Salum Madadi amesema kuwa ligi hiyo imemalizika kwa mafanikio makubwa licha ya kuwepo kwa baadhi ya changamoto ambazo shirikisho hilo litazifanyia kazi, huku akitaja changamoto moja wapo kuwa ni umri wa baadhi ya wachezaji kutokuwa sawa.

Madadi amesema miongonui mwa mafanikio yaliyopatikana katika ligi hiyo ni kupatikana na wachezaji 40 kwa ajili ya
kutengeza timu ya taifa ya vijana, pamoja na kupata funzo kuelekea kuwa na ligi kamili ya vijana.

"Ni kweli inawezekana kabisa kuna wachezaji ambao wamezidi umri, lakini katika hii cream ya wachezaji 40 tuliowachagua,
tutawafuatilia zaidi na tuna uhakika 20 tutakaowachagua watakuwa hawana tatizo la umri". Amesema

Rais wa TFF Jamal Malinzi akikabidhi kombe kwa nahodha wa Simba

Michuano hiyo imehitimishwa jana kwa kushuhudia vijana wa Simba wakitwaa ubingwa kwa kuifunga Azam kwa penati 5-3 baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 katika muda wa kawaida.

Kwa upande wake Rais wa TFF, Jamal Malinzi amesema kuwa wachezaji 40 bora kutoka katika mashindano hayo wataunda kikosi cha awali cha timu ya taifa ya U23 kwa ajili ya kufuzu fainali za Olimpiki Tokyo 2020