Jumanne , 21st Feb , 2017

Rapa Golden Jacob alimaarufu kama King Zillah kutoka Salasala amejitangaza rasmi kuwa yeye ni mfalme wa Freestyle bongo na kusema jambo hilo halina ubishi wowote ule

King Zillah

King Zillah amesema hayo kupitia mtandao wake wa twitter na kusema hakuna rapa ambaye anaweza kufanya mitindo huru kama yeye, Zillah anasema kigezo alichotumia ni kutokana na baadhi wa rapa kupewa nafasi ya kuonesha uwezo wao ndani ya dakika kumi za maangamizi ndani ya Planet Bongo, huku yeye akizitumia dakika zote kumi kufanya mitindo huru tofauti na wengine.

"Naamini wewe mwenyewe unajua kuwa mimi ni mfalme wa 'freestyle' hata ile dakika kumi za maangamizi pia zimeleta jibu juu ya hili, lakini pia utofauti wangu natengeneza freestyle na hits" alisema King Zillah 

Mbali na hilo Rapa Young Killer jana alifunguka na kusema kwa bongo yeye anamkubali zaidi Godzillah pamoja na Nikki Mbishi kwa 'freestyle' pia alikuwa akimuelewa marehemu Albert Mangwea na kusema hajawahi kumkubali Fid Q kwa 'freestyle' sababu hajawahi kumuona akifanya kitu hicho. 

Zitazame hapa dakika kumi za maangamizi za King Zillah, Fid Q, Nikki Mbishi, Young Killer pamoja na Chemical 

Zillah 
Fid Q
Nikki Mbishi 
Chemical
Young Killer