
Kamanda Magiligimba amesema katika oparesheni ya kupambana na madawa ya kulevya wamefanikiwa kuwa kamata watuhumiwa hao wakiwa na misokoto ya bangi 238 sawa na gramu 484 na kete 80 za Heroin sawa na gramu 160.
“Mbinu zilizotumika kuhifadhi Heroin ni mtuhumiwa aliamua kuficha kete kwenye matundu ya sabufa na kuanza kuuza kidogo kidogo na misokoto ya bangi ilifichwa kwenye begi dogo la nguo na kupuliziwa marashi ili kuzia harufu ya bangi.”,amesema Kamanda Magiligimba.
Kamanda Magiligimba amesema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara baaada ya upelelezi kukamilika.