Jumatatu , 5th Mar , 2018

Uongozi wa Wilaya ya Nzega umewaonya baadhi ya wafanyabiashara wa Mkaa wanaofanya shughuli hiyo kinyume na utaratibu kwani hatua kali dhidi yao zitachukuliwa.

Onyo hilo limetolewa na mkuu wa Wilaya ya Nzega Godfrey Ngupula ambapo amesema hatua hiyo inalenga kunusuru misitu iliyopo wilayani humo ambayo inateketea kwa kukatwa na baadhi ya wafabiashara wa mkaa bila utaratibu maalum.

Aidha Mkuu huyo wa wilaya amewaomba wananchi kutafuta njia mbadala ya kupata nishati mbadala ya mkaa ikiwemo gesi ili kunusuru misitu wilayani humo ambayo ndio chanzo kikubwa cha mvua na kulinda uoto wa asili.

Nao baadhi ya Wananchi wakiwemo wanaojihusisha na biashara hiyo ya Mkaa wametoa maoni yao kwa kuitaka serikali kutafuta njia mbadala ya mkaa iikiwemo kusambaza gesi mpaka maeneo ya vijijini ili kudhibiti hali hiyo.